Sheikh Shaaban Mlewa alisifu juhudi kubwa zinazofanywa na Sheikh Salman Magwe katika kueneza elimu ya dini, malezi ya vijana, na kuimarisha umoja wa Waislamu nchini na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. “Sheikh Salman Magwe amekuwa ni mfano wa kuigwa katika kazi za kielimu, malezi ya kiroho, na uongozi wa kimaadili unaolenga kuleta umoja, amani, na maendeleo ya jamii ya Kiislamu,” alisema Sheikh Mlewa.

6 Oktoba 2025 - 20:25

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kilimanjaro, 5 Oktoba 2025 - Katika hafla iliyojaa furaha na heshima, Sheikh wa Mkoa wa Kilimanjaro, Sheikh Shaaban Mlewa, amemkabidhi Samahat Sheikh Salman Magwe, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ahlul-Bayt (as) Afrika Mashariki na Kati, Tuzo ya Malezi Mema, Uwalimu na Uongozi Bora.

Tukio hilo limefanyika katika mazingira ya kifahari ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro, likihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini, walimu wa vyuo vya kiislamu, pamoja na waumini kutoka maeneo tofauti ya nchi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo, Sheikh Shaaban Mlewa alisifu juhudi kubwa zinazofanywa na Sheikh Salman Magwe katika kueneza elimu ya dini, malezi ya vijana, na kuimarisha umoja wa Waislamu nchini na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

“Sheikh Salman Magwe amekuwa ni mfano wa kuigwa katika kazi za kielimu, malezi ya kiroho, na uongozi wa kimaadili unaolenga kuleta umoja, amani, na maendeleo ya jamii ya Kiislamu,” alisema Sheikh Mlewa.

Kwa upande wake, Sheikh Salman Magwe alitoa shukrani zake za dhati kwa heshima hiyo, akisisitiza kwamba tuzo hiyo ni motisha kwa viongozi wote wa dini kuendelea kutumikia jamii kwa moyo wa ikhlasi na upendo.

"Tuzo hii si yangu peke yangu, bali ni ya wale wote wanaoshirikiana nami katika safari ya kutoa elimu, malezi bora, na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as) kwa hekima na huruma," alisema Sheikh Magwe.

Taasisi ya Ahlul-Bayt (as) Afrika Mashariki na Kati imekuwa ikijulikana kwa mchango wake mkubwa katika kuandaa wanazuoni, kueneza elimu ya dini, na kutekeleza miradi ya kijamii inayolenga kuinua ustawi wa Waislamu na jamii kwa ujumla.

Your Comment

You are replying to: .
captcha